Waziri Aweso amteua CPA Sais Andongile Kyejo kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa MORUWASA

DODOMA-Waziri wa Maji, Jumaa Hamidu Aweso terehe 22 Februari 2025 amefanya mabadiliko ya kiutendaji katika Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Morogoro (MORUWASA).
Waziri Aweso kwa mamlaka aliopewa na Sheria ya Huduma za Maji na Usafi wa Mazingira Na. 5/2019 amemteua,CPA Sais Andongile Kyejo kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa MORUWASA.

Ndugu Kyejo alikuwa ni Mkurugenzi wa Fedha Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Dar Es Salaam (DAWASA) na atachukua nafasi ya Mhandisi Tamimu Katakweba aliyekua Mkurugenzi Mtendaji wa MORUWASA.

Aidha,Waziri Aweso amemuelekeza Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji,Mhandisi Mwajuma Waziri kuunda timu maalumu ya wataalamu watakaofanyia kazi changamoto za hali ya huduma ya upatikanaji wa maji Manisapaa ya Morogoro na maeneo yote yanayohudumiwa na MORUWASA katika kipindi ambacho utekelezaji wa mradi mkubwa wa maji unaendelea.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news