Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), akiteta jambo na Mbunge wa Viti Maalum, na Mwenyekiti wa Chama cha Wabunge cha Kutokomeza Malaria Tanzania (TAPAMA), Mhe. Riziki Lulida, nje ya Jengo la Hazina, Jijini Dodoma, baada ya kukutana na kufanya mazungumzo na Ujumbe wa Asasi ya Kiraia inayojihusisha na masuala ya watu Wenye Ulemavu (SWAUTA), ambapo pamoja na mambo mengine, Mhe. Dkt. Nchemba aliwahakikishia utayari wa Serikali kuendelea kuyasaidia Makundi Maalumu kufikia ndoto yao ya kujikwamua kiuchumi kupitia mipango na ruzuku inayotolewa na Serikali kupitia Bajeti Kuu.
