DODOMA-Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), amekutana na kufanya mazungumzo na Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI), Mhe. Zainab Katimba (Mb), Treasury Square jijini Dodoma ambapo wamejadiliana kwa kina namna ya kuboresha miundombinu ya barabara inayosimamiwa na Wakala wa Barabara Vijijini (TARURA) ili kurahisisha usafiri na usafirishaji wa abiria na bidhaa.
Kikao hicho kilimhusisha pia Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, Naibu Katibu Mkuu -TAMISEMI (Miundombinu), Mhandisi Rogatus Mativila, Kamishna wa Bajeti, Wizara ya Fedha, Bw. Meshack Anyingisye, Mkurugenzi wa Miundombinu OR-TAMISEMI, Bw. Gilbert Mwoga na Mhasibu Mkuu wa TARURA, CPA Jacob Nyaulingo.