Waziri Jafo aunda timu Kariakoo

DAR-Waziri wa Viwanda na Biashara,Mhe Dkt. Selemani Jafo ameunda Timu ya watu 15 kwa ajili ya kufuatilia changamoto inayowakumba wafanyabiashara wa Kariakoo ya wawekezaji wageni wanaokuja nchini na ajenda ya uwekezaji kinyume chake wanajishughulisha na biashara za rejereja (Wamachinga) na kuathiri uchumi wa wafanyabiashara wazawa.
Dkt. Jafo alitangaza Timu hiyo jijini Dar es Salaam wakati akiongea na Uongozi wa Jumuiya ya Wafanyabiashara wa Kariakoo ambapo kuhusu utatuzi wa Changamoto mbalimbali zilizopo katika Soko hili ili kuliwezesha kufanya kazi kwa ufanisi.

Dkt. Jafo alifafanua kuwa Timu hiyo inayojumuisha wajumbe kutoka Taasisi mbalimbali katika sekta ya umma na binafsi itafanya kazi kwa siku 30 na itaanza kazi hivi karibuni ikiongozwa na Mwenyekiti wao Edda Tandi Luoga Mkuu wa Chuo cha Elimu ya biashara (CBE)

Aidha, Dkt. Jafo akieleza majukumu ya timu hiyo amesema Timu hiyo inatakiwa kufanya utafiti kwa kina kwa soko la kariakoo, kubaini ukubwa wa tazizo la wageni kupewa vibali na leseni za kufanya biashara nchini zinazoweza kufanywa na watanzania, kuchambua uhalali wa vibali na leseni zilizotolewa kwa wafanyabiashara wageni.

Aidha,Dkt. Jafo amesema Timu hiyo itafanya kazi ya kubaini sekta na aina ya biashara na maeneo yenye changamoto kwa wageni hapa nchini, kuchunguza utaratibu na upatikanaji wa nyumba za kufanyia biashara kwa wageni, kuchunguza udhaifu wa mfumo na uwezekano wa wageni kutumia njia zisizo rasmi kufanya biashara hapa nchini,

Aidha, timu hiyo inatakiwa kutoa mapendekezo ya hatua za haraka zitakazoweza kuchukuliwa na taasisi katika kudhibiti wageni wanaoingia kufanya biashara na ajira zinazostahili kufanywa na Watanzania.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news