DODOMA-Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi amekutana na viongozi wa Chama cha Wachapishaji wa Vitabu Tanzania (PATA) katika ofisi zake jijini Dodoma kwa ajili ya kuangalia fursa maridhawa katika kubadilishana uzoefu na kuimarisha sekta ya uandishi na uchapishaji wa vitabu Tanzania.
Katika kikao hicho Waziri Kabudi amewasisitiza chama hicho kutafsiri vitabu vilivyo katika lugha nyingine kuja katika Kiswahili fasaha na sanifu.
Pia, amewahamasisha kuchapisha vitabu vya hadithi fupifupi ambavyo vitapata soko katika nchi mbalimbali zinazoridhia ufundishwaji na ujifunzwaji wa Kiswahili.