Waziri Kombo afanya mazungumzo rasmi na Waziri wa Mambo ya Nje wa Hungary,wakubaliana kuimarisha ushirikiano

BUDAPEST-Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Mahmoud Thabit Kombo (Mb.) amekutana na kufanya mazungumzo rasmi na Waziri wa Mambo ya Nje na Biashara wa Hungary kwa lengo la kuimarisha ushirikiano baina ya Tanzania na Hungary.
Mazungumzo hayo yamefanyika katika Wizara ya Mambo ya Nje ya Hungary jijini Budapest.

Katika mazungumzo hayo, imetangaza rasmi nia yake ya kuipatia Tanzania Dola za Marekani milioni 55.1 sawa na bilioni 140 za Tanzania kwa ajili ya kutekeleza Mradi wa Usambazaji Maji wa Biharamulo.

Maeneo mengine ambayo imekubaliwa kuanzisha ushirikiano ni sekta ya biashara na uwekezaji, viwanda na teknolojia, elimu na kujengeana uwezo, kilimo, utalii, michezo, nishati na utunzaji wa mazingira, tiba na uzalishaji wa dawa, ufundishaji wa lugha ya Kiswahili nchini Hungary, uchukuzi na kuanzisha safari za ndege baina ya Tanzania na Hungary.

Kwa ajili ya kusimamia kwa karibu maeneo hayo ya ushirikiano, Hungary imetangaza uamuzi wake wa kufungua Ofisi ndogo za Ubalozi jijini Dar es Salaam ili kuratibu ushirikiano katika maeneo hayo. Kwa sasa Hungary inawakilishwa nchini kupitia Ubalozi wake wa Nairobi, Kenya.

Ofisi hizo za Ubalozi zinatarajiwa kukamilika na kuzinduliwa mapema mwezi Septemba mwaka huu.

Kwa upande wake Waziri wa Hungary alimshukuru Waziri Kombo kwa ziara hiyo ambayo imekuza zaidi ushirikiano baina ya Tanzania na Hungary.

Aidha, Waziri huyo alieleza kuwa ziara ya mwisho ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania nchini Hungary ilifanyika miaka 47 iliyopita. Hivyo ziara hii ni ishara kuwa Tanzania iko tayari kushirikiana na Hungary kwa manufaa ya pande zote mbili.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news