Waziri Kombo atembelea watengenezaji wa ndege nyuki (drones) za kilimo

BUNDAPEST-Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Mahmoud Thabit Kombo (Mb.) amefanya ziara katika Kampuni ya ABZ Innovation inayojihusisha na uzalishaji wa ndege zisizo na rubani ‘drones’ zinazotumika katika sekta ya kilimo.
Katika ziara hiyo Mhe. Waziri Kombo alipokea wasilisho kuhusu ndege hizo zinazozalishwa na kampuni ya ABZ Innovation ambazo zaidi hutumika katika kumwagilia mashamba, kunyunyizia dawa mashambani, kupuliza dawa ya kuua wadudu waenezao magonjwa kama vile mbu ili kupunguza na kudhibiti ugonjwa wa malaria.
Uwezo wa ndege hizo hutofautiana huku nyingine zikiweza kubeba lita 30 za maji na kumwagilia zaidi ya hekta 24 kwa saa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news