Waziri Lukuvi ampa kongole Mheshimiwa Waziri Mkuu

DODOMA-Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge na Uratibu Mheshimiwa William Lukuvi amemshukuru na kumpongeza Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muugano wa Tanzania Mheshimiwa Kassim Majaliwa kwa kuendelea kusimamia na kuratibu shughuli za Serikali.Waziri Lukuvi ametoa pongezi hizo wakati wa Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu uliofanyika Februari 7,2025 katika Ukumbi wa Ofisi hiyo Ngome jijini Dodoma.

Alisema kuwa kazi ya Waziri Mkuu kwa Mujibu wa Katiba ni kuratibu shughuli zote za Serikali na chini yake yupo Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati na watendaji wa Ofisi yake ambao wanatekeleza majukumu hayo kwa weledi na ufanisi mkubwa.
“Wakati wa uratibu wa shughuli za Maafa watendaji mmefanya kazi kwa ushirikiano Mkubwa chini ya Uongozi wa Mhe. Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na mambo yameenda vizuri nchi nzima,” alisema Waziri Lukuvi

Aidha alifafanua kuwa kazi ya Ofisi ya Waziri Mkuu ni kuratibu Serikali ili kuwafahamisha namna Serikali inavyoendelea kutekeleza majukumu na kuhudumia wananchi.

"...kwa kuwa tuna nafasi ya kupata taarifa na kuzifanyia uchambuzi ili kujulisha umma kwa njia mbalimbali ikiwemo vyombo vya habari basi tuendelee kuratibu vyema taarifa na kuzitoa kwa usahihi ndiyo jukumu letu kubwa na la msingi lazima tujipange ili ziweze kutoka kwa wakati alisema,” Waziri Lukuvi.
Naye Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Dkt. Jim Yonazi katika maneno ya utangulizi amesema Viongozi wa Ofisi ya Waziri Mkuu wamewatengeneza mazingira mazuri kwa watendaji kufanya kazi kwa furaha na amani.

Pia ameahidi kuimarisha ushirikiano miongoni mwao ili kuyafikia maelengo ya ofisi na Serikali kwa ujumla.

"Tuimarishe ushirikiano miongoni mwetu ili kazi zetu ziende kwa wepesi na ufanisi kwa kuamini kila mmoja ana mchango chanya kuhakikisha malengo yanatimia," alisema Dkt. Yonazi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news