DODOMA-Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-TAMISEMI Mhe. Mohamed Mchengerwa amekutana na wawakilishi wa Kampuni ya Straling Holding ya Abu Dhabi na kujadili namna bora ya ujenzi wa mji mpya wa kisasa katika Jiji la Dar es Salaam.

Mhe. Mchengerwa amefanya kikao kazi na wawekezaji hao ili kuwa na uelewa wa pamoja juu ya shughuli wanazozifanya, ili kuona kama kuna haja ya kushirikiana nao katika ujenzi wa mji mpya wa kisasa katika jiji la Dar es Salaam kwa kuzingatia maslahi mapana ya taifa.