LINDI-Waziri Mkuu na Mbunge wa Jimbo ya Ruangwa Mheshimiwa Kassim Majaliwa leo Februari 22, 2025 ameshiriki katika mazishi ya marehemu Bi. Asina Omary Nyimbilile mkazi wa Kata ya Nkowe, Ruangwa mkoani Lindi.

Bi. Asina amezikwa katika makaburi ya jumuiya yaliyopo katika kata ya Nkowe.
Maziko hayo pia yamehudhuriwa na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Lindi Ndugu Hassan Jarufu, Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa, Hassan Ngoma na Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Ruangwa Ndugu Ibrahim Ndoro.