Waziri Mkuu kuzindua Kampeni ya Kitaifa ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia mkoani Lindi

LINDI-Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Februari 19, 2025 atazindua kampeni ya Kitaifa ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia katika mkoa wa Lindi, kwenye viwanja vya Madini, Ruangwa mkoani humo.
Lengo la Kampeni hiyo ni kuwafikia wananchi wenye uhitaji na wasio na uwezo wa kumudu gharama za huduma za kisheria. Pia kampeni hiyo itawezesha kupata utatuzi wa migogoro kwa njia mbadala, kuongeza uwajibikaji kwa watendaji na kuimarisha umoja na mtangamano miongoni mwa jamii.
Mpaka sasa kampeni hiyo imefika katika mikoa 16 na kuhudumia wananchi zaidi ya milioni 1. Kaulimbiu ya kampeni hiyo ni “Msaada wa Kisheria kwa Haki, Usawa Amani na Maendeleo”.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news