KAGERA-Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Deogratius Ndejembi ametembelea na kujionea eneo linalotarajiwa kujengwa kitega uchumi kwa ajili ya wafanyabiashara wadogo (wamachinga) ambapo zaidi ya Sh. Bilioni 9 kukamilisha azma hiyo ya Serikali.
Waziri Ndejembi amesema hayo baada ya kutembelea la makaburi ya Kishenge Februari 11, 2025 Manispaa ya Bukoba mkoani Kagera ambapo wanatarajia kuhamishia makaburi hayo eneo la Buhembe mjini hapo.
Ni jambo kubwa ambalo linaenda kufanyika, ni fedha nyingi ambayo serikali yetu hii inayoongozwa na Dkt. Samia Suluhu Hassan imetenga Zaidi ya bilioni 9 kwa ajili ya ujenzi wa kitenga uchumi hapa manispaa ya Bukoba.
Waziri Ndejembi ameongeza kuwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan anaangalia maslahi ya wananchi wake anaowaongoza na kuona ni namna gani anawakwamua wafanya biashara ndogondogo kufanya biasha zao kwa usalama zaidi.
“Yalipokuja maombi ya kutwaa eneo hili la makaburi, ilitaarifiwa makaburi yanayopendekezwa kuhamishwa ni 3600, ni namba kubwa. Tukasema muhimu sisi wizara ya Ardhi kuja kujionea wenye,” amesema Waziri Ndejembi.
Waziri Ndejembi amesema kabla ya kuanza zoezi hili, kuna umuhimu wa viongozi wa Manispaa ya Bukoba kutoa taarifa na kuwatangazia watu waliozika ndugu zao hapo wajue kusudio la kuhamisha makaburi hayo na kusisitiza kupewa uhakika wa eneo ambalo limetengwa kuhamishia makaburi hayo kwa kuwasilisha nyaraka za umiliki wa eneo hilo ofisini kwake.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa huo Fatma Mwassa amesema fedha zinazotarajiwa kutumika kwenye ujenzi huo kwa ajili ya ujenzi wa eneo la wamachinga zaidi ya Sh. Bilioni 9 tayari zimetolewa.
