Wizara ya Maendeleo ya Jamii Zanzibar yasaini Makubaliano ya Ushirikiano (MoU) na Qatar Foundation

ZANZIBAR-Wizara ya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Zanzibar imesaini Makubaliano ya Ushirikiano (MoU) na Wakfu wa Qatar (Qatar Foundation).
Hafla hiyo imefanyika leo Februari 17,2025 huko Kinazini jijini Zanzibar ambapo wizara imewakilishwa na Katibu Mkuu, Abeida Rashid Abdallah huku kwa upande wa Qatar Charity wakiongozwa na Mkurugenzi Mkazi nchini Tanzania,Amjad Altahhan.

Katibu Mkuu Abeida Rashid Abdallah akizungumza katika hafla hiyo,ameushukuru Wakfu wa Qatar kwa juhudi zao za kuunga mkono masuala ya Ustawi wa Jamii Zanzibar.

"Eneo letu la ushirikiano linajikita katika maeneo mawili Ustawi wa Jamii ikiwemo udhamini wa yatima, familia za watoto wahitaji katika masuala ya elimu, afya na fedha."
Amesema, wakfu huo pia unashiriki kuwajengea uwezo wafanyakazi wanaofanya kazi katika jamii na wadau wa ulinzi wa watoto nchini.

"Eneo lingine ni Maendeleo ya Jamii ambalo linajumuisha uwezeshaji wa kiuchumi kwa watu binafsi na familia, kuboresha hali ya maisha na mengineyo."

Amesema,Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto ni moja ya taasisi za Serikali ya Zanzibar inayotekeleza majukumu ya kijamii ikiwemo kutunza watoto, yatima, wazee, watu walio katika hali ya uhitaji na familia zenye changamoto.
Katibu Mkuu huyo amesema,wizara hiyo inaongozwa kupitia sera, sheria na miongozo mingine ikiwemo Sera ya Ustawi wa Jamii ya Zanzibar ya mwaka 2014, Sera ya Jinsia ya mwaka 2016, Sheria ya Watoto Na. 6 ya mwaka 2011 na kanuni zake pamoja na Sheria ya Masuala ya Wazee ya mwaka 2020.

Ameongeza kuwa,wizara hiyo ina jukumu la kulinda jamii na kutoa msaada kwa wale walio katika hali ya uhitaji.

"Kwa mfano, tunasaidia familia maskini kifedha na wazazi wa watoto wenye changamoto, wazee kwa pensheni, elimu, matibabu na mahitaji mengine ya kila siku.
"Hata hivyo, msaada tunaotoa kwa wale wanaohitaji bado haukidhi mahitaji yao kikamilifu."

Wakati huo huo, Katibu Mkuu huyo ameishukuru Qatar Charity kwa kuanzisa makubaliano hayo ambayo wanaamini yatakuwa na matokeo chanya kwa jamii nchini huku akiahidi ushirikiano wa kutosha.

Kwa upande wa Qatar Foundation wameahidi ushirikiano zaidi katika kustawisha Ustawi wa Jamii na kuchochea kasi ya maendeleo katika jamii Zanzibar.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news