ZANZIBAR-Katika kuadhimisha Sikukuu ya Eid El Fitri, Wizara ya Biashara na Maendeleo ya Viwanda imeandaa Tamasha la Biashara la Eid El Fitri kwa ajili ya wajasiriamali hivyo tunaombwa kuchangamkia fursa ya kushiriki kwenye tamasha hilo litakalofanyika kuanzia tarehe 30 Machi hadi 4 Aprili 2025, katika viwanja vya maonesho Dimani, Zanzibar.
Tamasha hili linatarajiwa kuwa jukwaa muhimu la kukuza biashara, kuonyesha bidhaa na huduma mpya, na kuvutia wateja kutoka maeneo mbalimbali.
Lengo kuu ni kutoa nafasi kwa wajasiriamali
kuonyesha ubunifu wao, kuimarisha uhusiano wa kibiashara, na kufungua milango ya fursa za
kibiashara kwa wageni na wakazi wa Zanzibar.