Yanga SC yaachana na Kocha Sead Ramovic yampa kandarasi Miloud Hamdi

DAR-Klabu ya Yanga SC imemtangaza Miloud Hamdi mwenye uraia wa Algeria na Ufaransa kuwa kocha wake mpya akichukua mikoba ya Sead Ramovic ambaye anaondoka klabuni hapo baada ya kuvunja mkataba na kocha Mjerumani huyo kwa makubaliano ya pande zote mbili.
Taarifa ya leo Februari 04, 2025 iliyotolewa na klabu hiyo imebainisha kuwa, Kocha Hamdi mwenye uzoefu mkubwa wa kufundisha soka akiwa amefanya kazi barani Ulaya, Asia na Afrika, anaungana na timu mara moja kuanza majukumu yake mapya.

Kocha huyo mbali na uzoefu alionao, pia ana mafanikio makubwa katika soka la Afrika akishinda taji la Ligi Kuu ya Algeria na kucheza Fainali ya Ligi ya Mabingwa barani Afrika msimu wa 2015-2016 akiwa na USM Alger.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news