DAR-Young Africans Sports Club (Yanga SC) imepunguzwa nguvu ya kuendelea kuwa kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara baada ya kutoka sare tasa dhidi ya JKT Tanzania.
Pengine hayo ni matokeo ambayo yaliwashangaza wengi ikizingatiwa mabingwa hao watetezi wa ligi kuu wamekuwa wakiachia vichapo vya nguvu kwa timu mbalimbali.
Mtanange huo umepigwa Februari 10,2025
katika dimba la Meja Jenerali Isamuyo.
Aidha,kwa matokeo haya, Yanga wanabaki kileleni wakiwa na alama 46 ikiwa ni alama mbili mbele ya Simba ambao Februari 11,2025 watakuwa dimbani dhidi ya Prisons.