KIGOMA-Young Africans Sports Club (Yanga SC) imewatembezea kipigo kizito cha mabao 5-0 Mashujaa FC ikiwa ni mwendelezo wa michuano ya ligi kuu.
Mashujaa FC walipata kipigo hicho cha aibu Februari 23,2025 katika Dimba la Lake Tanganyika mkoani Kigoma.
Katika michuano hiyo ya Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara, Duke Abuya alifungua pazia la magoli dakika ya 32 ambalo lilidumu hadi tamati ya kipindi cha kwanza.
Hakika ya 48, Prince Dube alirejea nyavuni huku Khalid Aucho dakika ya 54 akipiga msumari wa tatu.
Clatous Chota Chama amefunga magoli mawili
dakika ya 74 na 83 ya kipindi cha pili cha mtanange huo.
Kwa matokeo hayo, Yanga SC wameendelea kujichimbia zaidi kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu bara pointi 55 baada ya mechi 21.