Zanzibar bado kuna fursa nyingi za uwekezaji-Rais Dkt.Mwinyi

ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt.Hussein Ali Mwinyi amesema, Zanzibar bado ina fursa nyingi za uwekezaji katika sekta mbalimbali na kuwakaribisha wawekezaji kutoka Saudi Arabia kuwekeza nchini.
Rais Dkt. Mwinyi ameyasema hayo leo alipozungumza na Wawekezaji na Wafanyabiashara wa Saudi Arabia waliofika Ikulu kuonana naye wakiwa katika ziara maalum Tanzania ya kubaini maeneo ya Ushirikiano na Uwekezaji pamoja na Biashara.
Aidha,Rais Dkt.Mwinyi amezitaja sekta nyingine ambazo zina fursa za Uwekezaji ni Kilimo, Mafuta na Gesi na Miundombinu na kuushukuru Ujumbe huo kwa kuamua kuja Zanzibar kwani Ziara hiyo itafungua ukurasa mpya wa Ushirikiano wa baina ya nchi hizo mbili na kuwasisitiza kuwa Mabalozi wazuri wa kuzitangaza fursa ziliopo nchini kwao.

Naye Rais wa Shirikisho la Jumuiya za Wafanyabiashara wa Saudi Arabia Hassan Alhuwayz amesema wana nia ya dhati ya kuimarisha Ushirikiano na Zanzibar hususani katika masuala ya Biashara na Uwekezaji kwani tayari wamebaini kuwepo kwa fursa nyingi pamoja na kuvutiwa na Maendeleo yaliyofikiwa na Zanzibar na hali ya Amani iliopo.
Wakati huo huo Rais Dkt.Mwinyi alishuhudia Utiaji wa Saini wa Mikataba baina ya Zanzibar na Saudi Arabia ikiwemo Mkataba wa Ushauri kati ya Zanzibar na Kampuni ya Saudi Arabia African Investment and Development Company na Mkataba wa Ushirikiano baina ya Jumuiya ya kitaifa ya Wafanyabiashara wa Zanzibar (ZNCC) na Shirikisho la vyama vya Wafanyabiashara wa Saudi Arabia kwa lengo la kuimarisha Uwekezaji wa kimkakati na kukuza Uchumi wa Zanzibar.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news