ZMA yakutana na mabaharia Zanzibar

ZANZIBAR-Uongozi wa Mamlaka ya Usafiri Baharini Zanzibar (ZMA) umefanya kikao cha pamoja na Chama cha Mabaharia Zanzibar lengo ni kujadili maendeleo na mustakabali wa chama hicho cha mabaharia ambapo kumekuwa na changamoto ya kukosa mashirikiano kati ya chama hicho na mashirika mengine yanayohusiana na shughuli za kibaharia
Akizungumza katika kikao hicho Mwenyekiti wa chama hicho cha mabaharia Zanzibar,ndugu Omar Salum Seif amesema,kumekuwa na changamoto nyingi sana zinazoikabili taasisi yao ikiwemo kutoshirikishwa kwenye shughuli mbalimbali za kiserikali na kikanda zinazohusiana na masuala ya ubaharia.

Aidha, Mwenyekiti Omar amesema, kumekuwa na uwiano mdogo baina ya mabaharia wanawake wanaoajiriwa ukilinganisha na mabaharia wa kiume, jambo linalosababisha kuwepo kwa usalama mdogo kwa mabaharia wa kike wanapokua katika meli.

Hivyo inatakiwa kuzingatiwa uajiri wa baharia wanawake ili kuendana na kasi ya maendeleo ya wanawake kote duniani

Naye Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri Baharini (ZMA),ndugu Mtumwa Said Sandal amesema, wapo tayari kutoa mashirikiano mazuri kwa chama hicho cha mabaharia ili kuendeleza na kuunga mkono juhudi za Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt.Hussein Ali Mwinyi katika kukuza mashirikiano baina ya Mashirika ya Serikali na Taasisi Binafsi.

Kikao hicho kimeazimia kuendeleza ushirikiano baina ya Mamlaka ya Usafiri Baharini na Chama cha Mabaharia Zanzibar ili kutatua changamoto zinazoikumba taasisi hiyo.

Kikao hicho cha siku moja kimefanyika katika ukumbi wa mkutano wa ofisi ya Mamlaka ya Usafiri Baharini Malindi Mjini Magharibi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news