DODOMA-Mwenyekiti wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT), Mhe. Murshid Ngeze, amemuomba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kuridhia kurejesha Wiki ya Serikali za Mitaa ili kuendelea kutangaza mafanikio ya mamlaka hizo.

Hata hivyo, amesisitiza kuwa kurejeshwa kwa Wiki ya Serikali za Mitaa kutazipa halmashauri zote nchini jukwaa rasmi la kuonyesha maendeleo na mafanikio katika maeneo yao.