Askari akamatwa kwa kushiriki uchotaji wa mafuta ajali ya lori

TABORA-Jeshi la Polisi Mkoa wa Tabora linamshikilia askari wa usalama barabarani, WP 8032 PC Victoria kutoka Wilaya ya Igunga, kwa kushiriki katika uchotaji wa mafuta kutoka kwa lori lililopata ajali.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Richard Abwao alieleza kuwa, askari huyo alifika katika eneo la ajali, lakini badala ya kudhibiti wananchi waliokuwa wakichota mafuta kutoka kwa lori lililoharibika, alionekana akitoa dumu kwa mmoja wao ili aendelee kuhifadhi mafuta hayo.

"Askari huyu hajazingatia taratibu na maadili ya kazi yetu kwa sababu badala ya kuonya wananchi, yeye anashiriki."

Ajali hiyo ilitokea katika Kijiji cha Igogo, barabara ya Igunga-Nzega, ambapo lori la mafuta liligonga kwa nyuma lori la mahindi, kisha kupoteza mwelekeo na kugonga lori jingine ambapo polisi wanaendelea na uchunguzi zaidi kuhusu tukio hili.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news