DAR-Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) limetangaza kuandama kwa mwezi leo Jumapili Machi 30, 2025 hivyo sala ya Idd El Fitri itafanyika kesho Machi 31,2025.
“Muft na Sheikh Mkuu wa Tanzania Sheikh Abubakar Zubeir leo ameutangazia umma wa Kiislam Tanzania kwamba leo siku ya Jumapili mwezi umeandama na umeonekana maeneo mbalimbali nchini. hivyo kesho siku ya Jumatatu ni sikukuu ya Idd.”