BAKWATA yatoa taarifa ya Sikukuu ya Eid El-Fitri

DAR-Baraza Kuu la Waislamu wa Tanzania (BAKWATA) limetoa taarifa kwa Waislamu na wananchi wote kwa ujumla kuwa Sikukuu ya Eid El-Fitri itakuwa Machi 31,2025 au Aprili 01,2025 kutegemea na mwandamo wa mwezi.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu BAKWATA, Alhaj Nuhu Mruma imesema sherehe za Eid El-Fitri kitaifa kwa mwaka huu zitafanyika Mkoa wa Dar es salaam.
Aidha,sala ya Eid itaswaliwa katika Msikiti wa Mfalme Mohamed VI BAKWATA Makao Makuu Kinondoni kuanzia saa 1.30 asubuhi na kufuatiwa na Baraza la Eid litakalofanyika katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere kuanzia saa 09.00 mchana Inshallah, Mgeni rasmi katika Baraza la Eid atakuwa Rais Dk. Samia Suluhu Hassan.

“Kwa niaba ya Baraza Kuu la Waislamu wa Tanzania Mh. Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania Dr. Sheikh Abubakar Zubeir bin Ally Mbwana anawatakia Swaumu njema katika kumi la mwisho la mwezi Mtukufu wa Ramadhani na maandalizi mema ya Sikukuu ya Eid B-Fitri.

“Tunaomba Waislamu wote kuhudhuria kwenye Ukumbi kwa wingi na kwa wakati, Wabillahi Tawfiq.”

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news