DAR-Kamanda Lilian Byebalilo (BAWACHA) ameshambuliwa kwa kupigwa na watu wa Taskforce iliyopo chini ya Waziri Mweneviale (Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Ilala), shambulio hilo limepelekea Lilian kupoteza fahamu na kukimbizwa hospitali kwa ajili ya matibabu kwa muda wa takribani saa tano katika Hospitali ya JEMSA iliyopo Segerea.
Na kisha kupewa rufaa ya kupelekwa Hospitali ya Amana iliyopo Ilala kwa ajili ya hatua zaidi za matibabu na uchunguzi wa afya yake, hii ni mara ya pili kwa tukio la namna hii kutokea baada ya tukio lile la kwanza la kushambuliwa kwa mwenezi wa BAWACHA Taifa, Siglada Mligo.
Tags
Habari