LUSAKA-Benki Kuu ya Zambia (BoZ) leo Machi 31,2025 imetoa matoleo mpya ya sarafu yanayojumuisha noti sita na sarafu sita, katika mgawanyo wa Kwacha ya 500, K200, K100, K50, K20, na K10.
Vilevile imetoa sarafu sita Kwacha 5, K2, K1, 50N, 10N, na 5N.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa imebainisha kuwa,noti mpya na sarafu mpya za K5, K2, na K1 zina miundo mipya na vipengele vya usalama vilivyoimarishwa.