BoT yaendelea kusherehekea Siku ya Wanawake Duniani kwa kufanya shughuli mbalimbali za kijamii

DAR-Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imeendelea kusherehekea Siku ya Wanawake Duniani kwa kufanya shughuli mbalimbali za kijamii zinazoakisi mshikamano na mchango wa wanawake katika maendeleo ya taifa.
Katika maadhimisho hayo, mgeni rasmi, Naibu Gavana wa Uthabiti na Usimamizi wa Sekta ya Fedha, Bi. Sauda Msemo, aliwahimiza wanawake kuendelea kuwa mstari wa mbele katika kuchochea maendeleo ya kijamii na kushiriki kikamilifu katika ujenzi wa jamii yenye usawa na haki kwa wote.
Pia aliwashukuru wanawake wa BoT kwa juhudi zao za kuchangia jamii na kuhamasisha mshikamano kwa kusaidia wahitaji.

Katika hotuba yake, Bi. Msemo aliwasihi wanawake kuwa mabalozi wa haki, usawa, na uwezeshaji katika kila nyanja ya maisha. Alisisitiza umuhimu wa kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia misingi ya maadili, utu, na hekima.
Moja ya shughuli muhimu zilizofanywa na wanawake wa BoT ni kuchangia fedha kwa ajili ya kusaidia wahitaji, ambapo walifanikiwa kununua viti vya magurudumu 24.

Aidha, walichangia kiasi cha fedha kwa Taasisi ya Ali Kimara Rare Disease Foundation, ambayo inahudumia watoto wanaoishi na magonjwa adimu.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news