DODOMA-Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imeendesha semina kwa Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti kuhusu Utekelezaji wa Sera ya Kupunguza Matumizi ya Fedha Taslimu.
Ujumbe wa Benki Kuu katika semina hiyo uliongozwa na Mkurugenzi wa Benki Kuu wa Mifumo ya Malipo ya Taifa, Bi. Lucy Shaidi na wasilisho kufanywa na Meneja Msaidizi, Bw. Mushumbusi Mutashobya.
Wengine katika ujumbe huo walikuwa ni Meneja Msaidizi kutoka Kurugenzi hiyo upande wa leseni na sera, Bw. Fabian Kasole.

Wametaka wadau wote katika sekta ya fedha kushirikiana kuongeza matumizi ya fedha za kidijitali, pamoja na kupunguza gharama za matumizi hayo ya fedha katika kufanya malipo kwa huduma na bidhaa.
Ujumbe wa Wizara ya Fedha katika semina hiyo uliongozwa na Kamishna Msaidizi, Bi. Dionisia Mjema.