DAR-Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) limeuruhusu Uwanja wa Benjamin Mkapa uliopo Dar es Salaam kutumika kwa michezo ya robo fainali na nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika (CAF CL) na Kombe la Shirikisho Afrika (CAF CC) 2024/2025.

Uwanja huo umeruhusiwa kutumika baada ya ukaguzi uliofanywa na wakaguzi wa CAF hivi karibuni, kutokana na kufungiwa kwa kutokidhi vigezo vya CAF.
Aidha,licha ya uwanja huo kuruhusiwa kutumika, CAF inaendelea kufuatilia kwa karibu maboresho yanayoendelea uwanjani hapo.