Daraja la Muhoro ni mkombozi kwa wananchi Rufiji-Mchengerwa

PWANI-Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Mhe. Mohamed Mchengerwa, amesema ujenzi wa Daraja la Muhoro utaleta ukombozi kwa wananchi wa Kata ya Muhoro, ambao kwa muda mrefu wamekumbwa na changamoto za usafiri na hata kupoteza maisha wanapovuka Mto Rufiji.
Akizungumza wakati wa ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi huo, Mhe. Mchengerwa amemshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kufanikisha mradi huo wa kisasa wenye thamani ya zaidi ya Sh.Bilioni 17.
"Nimeridhishwa na kasi ya ujenzi, lakini nataka mkandarasi aongeze juhudi ili daraja likamilike ifikapo Julai 2025,” amesisitiza Waziri Mchengerwa.

Kwa mujibu wa Meneja wa Wakala wa Barabara Mijini na Vijijiji (TARURA) Mkoa wa Pwani, Mhandisi Leopold Runji, ujenzi umefikia asilimia 40, tayari nguzo nne kati ya sita zimekamilika na lina urefu wa mita tisa, hivyo litasaidia kuzuia mafuriko.
Nao, Wakazi wa Muhoro, Pili Lwambo na Mikidadi Omary, wameeleza furaha yao, wakisema daraja hilo litaepusha vifo vinavyosababishwa na mamba, kusaidia kina mama kujifungua hospitalini, na kurahisisha usafiri wa watoto kwenda shule.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news