DC Kaegele awataka wananchi wa Butiama kujitokeza kupata elimu ya fedha

NA JOSEPHINE MAJURA
WF

SERIKALI imewataka Wananchi wa Wilaya ya Butiama, mkoani Mara, kujitokeza kwa wingi kushiriki katika mafunzo ya elimu ya fedha ili kujiongezea maarifa yatakayowasaidia kusimamia vizuri rasilimali zao.
Mkuu wa Wilaya ya Butiama, Mhe. Moses Kaegele, akiteta jambo na Timu ya Wataalamu kutoka Wizara ya Fedha na Benki Kuu ya Tanzania (BoT), ambao walifika ofisini kwake kujitambulisha ili kuanza kutoa elimu ya fedha kwa wananchi katika maeneo mbalimbali wilayani humo. Kutoka kushoto ni Afisa Sheria Mwandamizi, Idara ya Ustawi na Huduma Jumuishi za Fedha, Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Bw. Ramadhani Myonga, Afisa Usimamizi wa Fedha, Idara ya Uendelezaji Sekta ya Fedha, Wizara ya Fedha, Bw. Stanley Kibakaya na Afisa Usimamizi wa Fedha, Idara ya Uendelezaji Sekta ya Fedha, Wizara ya Fedha, Bi. Elizabeth Mnzava.

Rai hiyo imetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Butiama, mkoani Mara, Mhe. Moses Kaegele, alipokutana na Timu ya Wataalamu kutoka Wizara ya Fedha na Taasisi zake, ambayo ipo mkoani Mara kutoa elimu ya fedha kwa makundi mbalimbali.
Mkuu wa Wilaya ya Butiama, mkoani Mara, Mhe. Moses Kaegele, akikabidhiwa kipeperushi na Afisa Usimamizi wa Fedha, Idara ya Uendelezaji Sekta ya Fedha, Wizara ya Fedha, Bw. Stanley Kibakaya, chenye mada mbalimbali ikiwemo mikopo na akiba ambazo zitafundishwa kwa wananchi wilayani humo.
Mkuu wa Wilaya ya Butiama, mkoani Mara, Mhe. Moses Kaegele, akizungumza alipokutana na Timu ya Wataalamu kutoka Wizara ya Fedha na Benki Kuu ya Tanzania (BoT), ambao walifika ofisini kwake kujitambulisha ili kuanza kutoa elimu ya fedha kwa wananchi katika maeneo mbalimbali wilayani humo.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Butiama, mkoani Mara, Bi. Mbuke, akikabidhiwa kipeperushi na Afisa Usimamizi wa Fedha, Idara ya Uendelezaji Sekta ya Fedha, Wizara ya Fedha, Bi. Elizabeth Mnzava, chenye mada mbalimbali ikiwemo mikopo na akiba ambazo zitafundishwa kwa wananchi wilayani humo.

“Kushiriki katika mafunzo haya kutawawezesha wananchi kuepuka changamoto za kifedha kama vile madeni yasiyolipika, matumizi mabaya ya fedha, na kutokuwa na akiba ya kutosha kwa dharura,”alisema Mhe. Kaegele.

Aliongeza kuwa wananchi wakijitokeza kwa wingi kushiriki katika mafunzo ya elimu ya fedha kutawasaidia kupata maarifa yatakayowawezesha kufanya maamuzi bora ya kifedha na kujenga maisha yenye utulivu na mafanikio.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Butiama, mkoani Mara, Bi. Mbuke, akizungumza alipokutana na Timu ya Wataalamu kutoka Wizara ya Fedha na Benki Kuu ya Tanzania (BoT), ambao walifika ofisini kwake kujitambulisha ili kuanza kutoa elimu ya fedha kwa wananchi katika maeneo mbalimbali ya Halmashauri hiyo.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Butiama, mkoani Mara, Bi. Mbuke Makanyanga, aliipongeza Wizara ya Fedha kwa kazi kubwa wanayofanya ya kuhakikisha kila mwananchi anafikiwa na elimu muhimu ya fedha ili waweze kusimamia vizuri fedha zao.
Mkuu wa Wilaya ya Butiama, mkoani Mara, Mhe. Moses Kaegele, akizungumza alipokutana na Timu ya Wataalamu kutoka Wizara ya Fedha na Benki Kuu ya Tanzania (BoT), ambao walifika ofisini kwake kujitambulisha ili kuanza kutoa elimu ya fedha kwa wananchi katika maeneo mbalimbali wilayani humo. Kutoka kulia ni Afisa Usimamizi wa Fedha, Idara ya Uendelezaji Sekta ya Fedha, Wizara ya Fedha, Bi. Elizabeth Mnzava, Afisa Sheria Mwandamizi, Idara ya Ustawi na Huduma Jumuishi za Fedha, Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Bw. Ramadhani Myonga na Afisa Usimamizi wa Fedha, Idara ya Uendelezaji Sekta ya Fedha, Wizara ya Fedha, Bw. Stanley Kibakaya.

Naye Afisa Usimamizi wa Fedha, Idara ya Uendelezaji Sekta ya Fedha, Wizara ya Fedha, Bi. Elizabeth Mnzava, alisema kuwa wakati wanaendelea na zoezi la utoaji elimu katika makundi mbalimbali wamekutana na malalamiko kutoka kwa wananchi ambao wamekopa maeneo mbalimbali kubadilishiwa mikataba na watoa huduma wasiowaminifu.

“Tumekutana na kesi mwananchi anasema kwenye mkataba aliosaini siku ya kwanza alikopa kiasi fulani, lakini anaporudi ofisini kutaka kuanza kufanya rejesho la kwanza anakuta mkataba mpya wenye kiwango kikubwa tofauti na alichokopa,” alisema Bi. Elizabeth.
Baadhi ya washiriki wa mafunzo ya elimu ya fedha wakazi wa Kijiji Kyankoma, Kata ya Nyamimange, Wilaya ya Butiama, mkoani Mara, wakiangalia filamu yenye mada mbalimbali ikiwemo masuala ya mikopo, akiba na uwekezaji wakati wa mafunzo ya elimu ya fedha yaliyotolewa na Wataalamu kutoka Wizara ya Fedha na Benki Kuu ya Tanzania (BoT) mkoani Mara.(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini WF, Butiama Mara).

Alifananua kuwa ni haki ya mkopaji kuomba nakala ya mkataba wa mkopo ili utumike kama ushahidi iwapo kutatokea kubadilishiwa kiwango cha mkopo, lakini nakala hiyo itamsaidia mkopaji kujua taarifa muhimu ya kiwango cha riba, kiasi cha rejesho kila mwezi na kiasi cha mkopo alichokopa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news