Dkt.Biteko akutana na Mtendaji Mkuu wa Climate Investment Funds

BRIDGETOWN-Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amekutana na kufanya mazungumzo na Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Climate Investment Funds (CIF) Bi. Tariye Gbadegesin Mjini Bridgetown, Barbados.
Mazungumzo hayo yamefanyika leo Machi 14, 2025 kando ya Mkutano wa Kimataifa wa kuhusu upatikanaji wa Nishati endelevu kwa wote (Energy ForAll).
Dkt. Biteko amesema kuwa, Wizara ya Nishati iko tayari kukuza ushirikiano na Taasisi hiyo ili kuunganisha juhudi za pamoja kuhakikisha matumizi ya nishati safi ya kupikia hususan maeneo ya Vijijini.
Aidha, Katika mazungumzo hayo yamehudhuriwa na Mshauri wa Rais Masuala ya Nishati Safi na Maendeleo ya Jamii, Mhe. Angellah Kairuki, Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Mha. Felchesmi Mramba pamoja na Balozi wa Tanzania nchini Cuba na mwakilishi katika eneo la Caribean, Mhe. Humphrey Polepole.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news