Dkt.Biteko awasili Barbados kunadi nishati safi Kimataifa

BRIDGETOWN-Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amewasili nchini Barbados kushiriki Mkutano wa Kimataifa kuhusu matumizi ya Nishati endelevu utakaofanyika katika jiji la Bridgetown kuanzia tarehe 12 hadi 14 Machi, 2025.
Katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Grantley Adams nchini humo, Dkt. Biteko amepokelewa na Waziri wa Nishati wa Nchi hiyo Mhe. Lisa Cummins pamoja na Balozi wa Tanzania nchini Cuba na mwakilishi katika eneo la Caribean, Mhe. Humphrey Polepole.
Aidha, Dkt. Biteko atashiriki katika majadiliano mbalimbali kuhusu matumizi ya Nishati endelevu kimataifa ikiwemo Nishati safi ya kupikia ambayo ni ajenda muhimu kwa ajili ya kuwakomboa wananchi dhidi ya matumizi ya nishati isiyokuwa safi.

Dkt. Biteko ameongozana na Mshauri wa Rais masuala ya Wanawake, Mhe. Angellah Kairuki, Waziri wa Maji, Nishati na Madini Zanzibar, Mhe. Shaib Hassan Kaduara na Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Mha. Felichesmi Mramba.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news