DAKAR-Rais mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete tarehe 24 Machi 2025, amewasilisha Ujumbe Maalum wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa Rais wa Jamhuri ya Senegal, Mhe. Bassirou Diomaye Faye katika Ikulu ya Rais huyo jijini Dakar, Senegal.