WINDHOEK-Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango amemwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Maombolezo ya Kitaifa na Ibada ya kumuaga aliyekuwa Rais na Baba wa Taifa la Namibia hayati Dkt. Sam Nujoma iliyofanyika katika Uwanja wa Michezo wa Uhuru uliopo jijini Windhoek nchini Namibia.

Maombolezo ya Kitaifa na Ibada ya kumuaga hayati Dkt. Nujoma yamehudhuriwa na Viongozi mbalimbali wa Bara la Afrika na Mataifa mbalimbali nje ya bara la Afrika.
Hayati Dkt. Sam Nujoma alifariki tarehe 08 Februari 2025 na Mazishi ya kiongozi huyo yanatarajiwa kufanyika tarehe 01 Machi 2025 katika Makaburi ya Mashujaa Jijini Windhoek nchini Namibia.