Dkt.Mwinyi afuturisha viongozi wa CCM

ZANZIBAR-Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Hussein Ali Mwinyi amejumuika na Wajumbe wa Kamati Kuu na Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi katika futari aliyoiandaa.
Hafla hiyo ya imefanyika katika Viwanja vya Ikulu Zanzibar, tarehe 22 Machi 2025.
Ameeleza kuridhika kukamilisha Sadaka ya Futari kwa mikoa yote mitano ya Zanzibar kwa mafanikio na kuwashukuru waumini wa Dini ya Kiislamu na wananchi kwa kuitikia mialiko yake kwa mahudhurio makubwa katika mikoa yote Unguja na Pemba.

Aidha, Dkt.Mwinyi ametumia fursa Hiyo kuwatakia Waumini vwa Dini ya Kiislamu na wananchi Sikukuu Njema ya Idd el fitr.
Rais Dkt. Mwinyi amekuwa na utaratibu wa kufutarisha kila Mwezi wa Ramadhani,  utaratibu aliouhitimisha leo kwa viongozi hao wa Chama Cha Mapinduzi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news