Dkt.Nchemba afanya mazungumzo na Kamishna mpya wa Kitengo cha Kudhibiti Fedha Haramu (FIU)

DAR-Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), amekutana na kufanya mazungumzo na Kamishna wa Kitengo cha Kudhibiti Fedha Haramu (Financial Intelligence Unit-FIU), Bw. Majaba Magana aliyefika kujitambulisha baada ya kuteuliwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, hivi karibuni, kuongoza Kitengo hicho kinachoshughulika, pamoja na mambo mengine, kudhibiti utakasishaji fedha haramu, kikao kilichofanyika katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha jijini Dar es Salaam, ambapo Mhe. Dkt. Nchemba, aliahidi kumpa ushirikiano Kamishna huyo wa FIU, ili aweze kutimiza majukumu yake kikamilifu.
Kikao hicho kilihudhuriwa pia na Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Hamad Hassan Chande, Mkurugenzi wa Idara ya Mipango, Wizara ya Fedha, Bw. Moses Dulle na Maafisa wengine waandamizi kutoka Kitengo hicho cha FIU na Wizara ya Fedha.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news