Dkt.Nchemba akutana na Mtakwimu Mkuu mpya wa Serikali

DAR-Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), amekutana na kufanya mazungumzo na Mtakwimu Mkuu Mpya wa Serikali, Dkt. Amina Msengwa, aliyefika kujitambulisha baada ya kuteuliwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, hivi karibuni, kuchukua nafasi ya aliyekuwa Mtakwimu Mkuu wa Serikali, Dkt. Albina Chuwa, ambaye amestaafu rasmi utumishi wa Umma, kikao kilichofanyika katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha jijini Dar es Salaam, ambapo Mhe. Dkt. Nchemba, alihidi kumpa ushirikiano Mtakwimu Mkuu huyo wa Serikali ili aweze kutimiza majukumu yake kikamilifu.
Kikao hicho kilihudhuriwa pia na Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Hamad Hassan Chande, na Viongozi wengine waandamizi kutoka Ofisi ya Taifa ya Mtakwimu (NBS), Mkurugenzi wa Idara ya Mipango, Wizara ya Fedha, Bw. Moses Dulle, na Maafisa kutoka Wizara ya Fedha.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news