Dkt.Nchemba ashiriki uzinduzi wa huduma za kidigitali Benki ya NBC

DAR-Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba (Mb), ameshiriki uzinduzi wa huduma za kidigitali za Benki ya NBC (NBC Kiganjani App) inayomwezesha mteja kupata huduma za kibenki kigigitali kwa kutumia simu za mkononi tukio ambalo, Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa alikuwa Mgeni Rasmi, lililofanyika katika Ukumbi wa The Super Dome, Masaki jijini Dar es Salaam.
Akimkaribisha, Mhe. Waziri Mkuu kuzungumza na kuzindua NBC Kiganjani App, Mhe. Dkt. Nchemba aliipongeza NBC kwa ubunifu walioufanya na kwamba hatua hiyo si tu kwamba inaimarisha maendeleo ya sekta ya benki, bali pia inaendana na dhamira ya serikali ya Awamu ya Sita, inayoongozwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ya kujenga uchumi jumuishi unaowezesha upatikanaji wa huduma za kifedha kwa wananchi wote.
Aidha, Mhe. Dkt. Nchemba, aliipongeza Benki hiyo kwa kudhamini Ligi Kuu ya Tanzania Bara (NBCPL) ambayo kupitia udhamini wao imekuwa na msisimko mkubwa na kuiwezesha Tanzania kupanda viwango na kuwa ligi namba 4 kwa Ubora baranı Afrika.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news