DODOMA-Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Sweden nchini, Mhe. Charlotta Ozaki Macias, aliyefika ofisini kwake Treasury Square jijini Dodoma, ambapo wamejadiliana kuhusu maendeleo ya Ujenzi wa Reli ya Kisasa - SGR unaondelea hapa nchini pamoja na Mradi wa Mabasi yaendayo haraka jijini Dar es Salaam (DART). Kikao hicho kiliwashirikisha Kamishna wa Idara ya Madeni-Wizara ya Fedha, Bw. Japhet Justine na Msaidizi wa Balozi huyo.