Dkt.Nchemba ateta na uongozi wa Mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi wa Afrika Mashariki

DAR-Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), amekutana na kufanya mazungumzo na Ujumbe kutoka Mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi wa Afrika Mashariki (EACOP), ukiongozwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mradi huo, Bw. Philippe Groueix, Kando ya Mkutano wa 11 wa Mafuta na Gesi unaozihusisha nchi za Afrika Mashariki unaoendelea katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam, ambapo wamejadiliana kuhusu maendeleo ya ujenzi wa mradi huo.
Kikao hicho kifupi kiliwashirikisha pia Kamishna wa Idara ya Sera, Wizara ya Fedha, Dkt. Johnson Nyella, Afisa Mwandamizi kutoka Idara ya Sera, Wizara ya Fedha, Bw. Justine Mlewa, Mkurugenzi Mtendaji wa EACOP, Bw. Guillaume Dulout, Mkuu wa masuala ya Utawala na Rasilimali Watu wa EACOP, Bw. Geofrey Mponda na Meneja Uhusiano wa Serikali wa Mradi huo Bi. Evelyne Amasi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news