MTUMIAJI Magazine, Jarida la Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA CCC) limedhamiria kuboresha viwango vya habari zake zinazowaelimisha watumiaji wa huduma za nishati na maji na kuwajuza haki zao.
Pichani, Bw. Derek Murusuri (kushoto), Mwezeshaji Kiongozi wa mafunzo hayo akishirikiana na Bw. Paul Mabuga (Kulia). Wengine wanao onesha vyeti ni Noela Ntiluvakule (katikati), Neema Nnko (wa pili kushoto na Catherine Charles (wa pili kulia).
Baraza hilo liliandaa mafunzo ya wiki mbili kuhusu umahiri katika uandishi wa habari, upigaji picha za kihabari, uzalishaji wa makala za picha mnato na uhabarishaji wa kidigiti.
Bw. Derek Murusuri, Mwezeshaji Kiongozi wa mafunzo ya umahiri (katikati) akimkabidhi cheti, Bi. Neema Nnko wa EWURA CCC, Mkoa wa Manyara. Kushoto ni Mwezeshaji mwenza, Bw. Paul Mabuga. (Picha kwa hisani ya EWURA CCC).

Bw. Derek Murusuri (kushoto), Mwezeshaji Kiongozi wa mafunzo ya umahiri akishirikiana na Bw. Paul Mabuga (hayuko pichani), akimkabidhi cheti cha kuhudhuria mafunzo hayo yatakayoboresha habari za Mtumiaji Magazine, Bi. Catherine Charles wa EWURA CCC, Mkoa wa kikazi wa Ilala, Dar es Salaam (Picha kwa hisani ya EWURA CCC).
Mafunzo hayo yaliyofanyika katika Manispaa ya Morogoro, yamefungwa rasmi leo.