DAR-Ninakumbuka, viongozi walipokuwa Gerezani tulifanya fundraising siku tatu tukapata pesa.
Hao viongozi wa chama wakiongozwa na Tundu Lissu wajiulize leo mbona hawapati wachangiaji? Badala yake wanajaza walinzi ukumbini tu.
Wanaishia kutudhalilisha tu, kwamba Makao Makuu watu wanalipwa kidogo sana, wakati wa kampeni walisema uongo mkubwa sana kwamba tulilipwa mamilioni.
Kuna aina fulani ya maumivu naipata,ila watavuna walichopanda muda ni dawa sahihi sana sana.
Ni jambo la kushangaza GSM Foundation ndani ya saa chache wamepata zaidi ya shilingi milioni 925, lakini Tone Tone pengine kwa siku kadhaa hawajafikisha hata shilingi milioni 100.
Hii, inadhirisha kuwa, kuna mahali kama chama tumekwama na wananchi wengi wametuchoka. Tujitafakari.
Tags
Habari