Kahawa ya Tanzania kukuza ushirikiano wa kiuchumi baina ya Tanzania na Italia

ROME-Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Mahmoud Thabit Kombo (Mb.) ameshiriki katika Mdahalo wa Wadau wa kukuza mnyororo wa thamani wa kahawa inayozalishwa barani Afrika uliofanyika pembezoni mwa Mkutano wa Mpango wa Mattei kwa Afrika na Lango la Kimataifa (The Mattei Plan for Africa and the Global Gateway) uliofanyika jijini Roma, Italia.
Mkutano huo ulihudhuriwa na wadau mbalimbali ikiwemo serikali ya Italia, Umoja wa Ulaya, kampuni kubwa za kahawa zikiwemo Illy na Lavazza, taasisi za fedha kama IFC na CDP, na wawakilishi kutoka FAO na IFAD.

Akizungumza katika Mkutano huo, Mhe. Waziri Kombo ametoa wito kwa wadau hao kuongeza uwekezaji katika mnyororo wa thamani wa zao la kawaha barani.
“Kukiwa na ustawi barani Afrika, tunaweza kutatua changamoto za hali ya hewa kwani misitu mikubwa barani Afrika inatumika kama nyenzo muhimu ya kunyonya kaboni na kwamba kuongezeka kwa uzalishaji wa kahawa kunaweza kuongeza nguvu katika kulinda mazingira lakini pia kutengeneza fursa za ajira kwa vijana.”

Mhe. Kombo alieleza mazingira rafiki ya uwekezaji katika zao la kahawa nchini, na kuwakaribisha wadau kuwekeza katika uzalishaji na uongezaji thamani wa zao linalopatikana kwa wingi nchini hali itayosaidia kuinua kipato cha wakulima. “Lavazza na Illy kila mara mnaongelea punje ya kahawa kwenda kinywaji, hamzungumzii kutoka ardhini hadi kuwa punje kwani usipokuwa na punje hakuna Lavazza hakuna Illy.
“Msiwe wanasiasa. Tuweke mpango kazi, tuweke ratiba ya utekelezaji. Tuweke ratiba ya ukamilishaji. Na hili linaweza kufanyika,” amesisitiza Mhe. Kombo.

Aidha, Katibu Mtendaji wa Shirika la Kahawa la InterAfrican, Solomon Rutega ameipongeza Tanzania kwa kufanikisha Mkutano wa Kahawa wa G25 ambao maazimio yake ya kuliongezea thamani zao la kahama kuanzia kwenye kilimo, uchakataji, uokaji wa mbegu hadi kumfikia mtumiaji wa mwisho vinalandana na maazimio ya ushirikiano wa Italia na Afrika katika zao la kahawa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news