Kamati ya Bunge yapitisha Mpango na Bajeti ya Ofisi ya Rais-Utumishi na taasisi zake kwa Mwaka wa Fedha 2025/26

NA VERONICA MWAFISI

KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria imepitisha Mpango na Bajeti ya Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora pamoja na taasisi zake kwa Mwaka wa fedha 2025/26 baada ya kupitia mafungu yote yaliyo chini ya ofisi hiyo na kujiridhisha.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akiwasilisha taarifa ya Utekelezaji wa Mpango na Bajeti kwa Mwaka wa Fedha 2024/25 pamoja na Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha 2025/26 kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria.

Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria, Mhe. Florent Kyombo amezungumza hayo leo tarehe 27 Machi, 2025 katika Ukumbi wa Mikutano wa Bunge jijini Dodoma alipokuwa akikaimu nafasi ya Mwenyekiti wa Kamati hiyo mara baada ya Wajumbe wa Kamati kujadili na kuridhia taarifa ya Utekelezaji wa Mpango na Bajeti kwa Mwaka wa Fedha 2024/25 pamoja na Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha 2025/26 ya Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Utawala Bora.
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria, Mhe. Florent Kyombo akiongoza kikao kazi cha kamati yake na Watendaji wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kiliyolenga kupokea na kujadili taarifa ya Utekelezaji wa Mpango na Bajeti kwa Mwaka wa Fedha 2024/25 pamoja na Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha 2025/26.
Sehemu ya Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Utawala, Katiba na Sheria wakifuatilia taarifa ya Utekelezaji wa Mpango na Bajeti kwa Mwaka wa Fedha 2024/25 pamoja na Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha 2025/26 iliyokuwa ikiwasilishwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene (hayupo pichani) wakati wa kikao kazi kilichofanyika katika Ofisi za Bunge jijini Dodoma.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akifafanua baadhi ya hoja zilizowasilishwa na wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Utawala, Katiba na Sheria wakati wa kikao kazi kilicholenga kuwasilisha taarifa ya Utekelezaji wa Mpango na Bajeti kwa Mwaka wa Fedha 2024/25 pamoja na Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha 2025/26.
Sehemu ya Watendaji wa Taasisi zilizopo chini ya Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora wakiwa katika kikao kazi cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria kilicholenga kupokea na kujadili taarifa ya Utekelezaji wa Mpango na Bajeti kwa Mwaka wa Fedha 2024/25 pamoja na Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha 2025/26.
Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria Mhe. Abeid Ramadhani (katikati) akiwasilisha hoja kwa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora wakati wa kikao kazi cha Kamati na ofisi hiyo kilicholenga kupokea na kujadili taarifa ya Utekelezaji wa Mpango na Bajeti kwa Mwaka wa Fedha 2024/25 pamoja na Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha 2025/26.
Sehemu ya Wakurugenzi na Watendaji wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora wakiwa katika kikao kazi cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria, na Watendaji wa ofisi hiyo kiliyolenga kupokea na kujadili taarifa ya Utekelezaji wa Mpango na Bajeti kwa Mwaka wa Fedha 2024/25 pamoja na Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha 2025/26.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene (kulia) akiteta jambo na Katibu Mkuu wa ofisi yake Bw. Juma Mkomi (kushoto) wakati wa kikao kazi cha kuwasilisha kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria taarifa ya Utekelezaji wa Mpango na Bajeti kwa Mwaka wa Fedha 2024/25 pamoja na Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha 2025/26.
Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma, Bw. Mick Kiliba akijibu hoja kuhusu ajira iliyowasilishwa na Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria wakati wa kikao kazi cha kamati hiyo na Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora na taasisi zake kilicholenga kupokea na kujadili taarifa ya Utekelezaji wa Mpango na Bajeti kwa Mwaka wa Fedha 2024/25 pamoja na Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha 2025/26.
Sehemu ya Wakurugenzi na Watendaji wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora wakifuatilia maoni yaliyokuwa yakitolewa na Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Utawala, Katiba na Sheria wakati wa kazi cha Kamati na ofisi hiyo kilicholenga kupokea na kujadili taarifa ya Utekelezaji wa Mpango na Bajeti kwa Mwaka wa Fedha 2024/25 pamoja na Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha 2025/26.
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria, Mhe. Florent Kyombo (kushoto) akisikiliza fafanuzi za hoja mbalimbali zilizotolewa na wajumbe wa Kamati yake kwa Watendaji wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora wakati wa kikao kazi kilicholenga kupokea na kujadili taarifa ya Utekelezaji wa Mpango na Bajeti kwa Mwaka wa Fedha 2024/25 pamoja na Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha 2025/26. Kulia kwake ni katibu wa Kamati hiyo, Bi. Ganjatuni Abel.

“Kamati imejadili na kuridhia kupitisha Mpango na Bajeti ya Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora pamoja na taasisi zake kwa Mwaka wa fedha 2025/26, niwapongeze kwa maandalizi mazuri yenye uwazi, Kamati inawaasa kuwa na matumizi mazuri ya fedha pale zitakapopitishwa katika vikao vya Bunge la Bajeti ambapo tunaamini mtafikia malengo ya kuwatumikia watanzania kwa maendeleo ya nchi.” Mhe. Kyombo amesema.

Kwa upande wake, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene ameishukuru Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria, kwa kuwa na majadiliano mazuri na ofisi anayoiongoza ambayo wanaamini yatawasaidia kwa kiasi kikubwa katika utekelezaji wa majukumu yao kupitia bajeti hiyo.

“Mhe. Mwenyekiti, nitoe shukrani za dhati kwa niaba ya ofisi ninayoiongoza mara zote tumepokea maoni, ushauri na michango mbalimbali kutoka katika Kamati yako inayolenga kuboresha Utumishi wa Umma nchini kwa lengo la kutimiza azma ya Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuwa na Utumishi wa Umma uliotukuka.
Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Juma Mkomi akitoa neno la shukrani kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria mara baada ya kumaliza kikao kazi cha Kamati na Watendaji wa ofisi hiyo kilicholenga kupokea na kujadili taarifa ya Utekelezaji wa Mpango na Bajeti kwa Mwaka wa Fedha 2024/25 pamoja na Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha 2025/26.
Sehemu ya Maafisa na Watendaji wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora wakiwa katika kikao kazi cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria, na Watendaji wa ofisi hiyo kiliyolenga kupokea na kujadili taarifa ya Utekelezaji wa Mpango na Bajeti kwa Mwaka wa Fedha 2024/25 pamoja na Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha 2025/26.
Sehemu ya Wakurugenzi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora wakiwa katika kikao kazi cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria, na Watendaji wa ofisi hiyo kiliyolenga kupokea na kujadili taarifa ya Utekelezaji wa Mpango na Bajeti kwa Mwaka wa Fedha 2024/25 pamoja na Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha 2025/26.

Akitoa neno la shukrani kwa niaba ya ofisi hiyo, Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bw. Juma Mkomi amesema Kamati hiyo imekuwa msaada mkubwa wa kuiongoza Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Utawala Bora kwa kuwapatia maarifa mengi kutoka kwa Wajumbe wote wa Kamati hiyo yenye kuboresha utendajikazi.

Mpango na Bajeti ya Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora na taasisi zake kwa Mwaka wa fedha 2025/26 umezingatia Dira ya Taifa ya Maendeleo ya 2025, Maelekezo ya Ilani ya CCM kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2020 na Mpango wa Tatu wa Taifa wa Maendeleo wa Miaka Mitano (2021/22-2025/26).

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news