Kazi Iendelee na Mama Samia wamuangukia Rais Dkt.Samia

DAR-Mtandao wa Maendeleo ya Sanaa na Utamaduni Tanzania (MMASUTA) kupitia kikundi chake cha Sanaa za Maigizo kinachoitwa ‘Kazi Iendelee na Mama Samia’, wamemuomba Rais Samia Suluhu Hassan kuwashika mkono katika kunadi miradi ambayo imetekelezwa na Serikali ya Awamu ya Sita, hususan wakati huu wa kuelekea kwenye Uchaguzi Mkuu, Oktoba mwaka huu.
David Msuya ambaye ni Mwenyekiti wa MMASUTA, amebainisha hayo leo jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari na kufafanua kwamba kikundi hicho kinawasanii wachanga ambao tayari wameshiriki katika kazi nyingi za kuiunga mkono Serikali katika mikoa mbalimbali nchini.

"Mara kadhaa tunapopata nafasi tunafanya shughuli mbalimbali za kuiunga mkono Serikali ikiwemo kufanya usafi katika Zahanati ambazo ni sehemu ya miundombinu ya afya ambayo imejengwa na Serikali yetu chini ya Rais Dkt.Samia, na kutokana na kuwa uzoefu huo tunamuomba Mama yetu atushike mkono nasi tuwe sehemu ya kutangaza miradi ambayo imetekelezwa chini ya uongozi wake,"amesema.
Ameongeza kuwa,wakati wa mafuriko wilayani Kilosa mkoani Morogoro yakiwa yametokea nao walikuwa sehemu waliofika kwa ajili ya kusaidia shughuli kadhaa za kibinadamu, hivyo wananaamini ikiwa watapatiwa nafasi ya kujumuika katika mikutano ya kiserikali na kichama wataweza kunadi vema mafanikio ya miradi iliyotekelezwa na Serikali ya Awamu ya Sita.

“Wasanii mnaowaona hapa leo wanavipaji vya aina tofauti tofauti kama vile uchezaji wa ngoma za asili, uigizaji, utunzi wa mashairi, ngonjera na uigizaji wa maigizo hivyo tukishirikishwa ipasavyo katika kazi mbalimbali za Serikali tutaweza kuzitangaza vyema kupitia vipaji wasanii hawa,” amesema Msuya.
Msuya alisema wasanii hao wanaimani na Mwenyekiti wa CCM Taifa ambaye pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, Katibu Mkuu wa CCM, Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi, Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM, Amos Makalla na wengineo.

Alisema wasanii hao chipukizi wamekaa na kutafakari na kuamua kumuomba Rais Samia awaweke katika timu ya itakayoshriki katika majukwaa yote ya kiserikali na kichama kwa pamoja kutangaza kazi ambazo zimetekelezwa na ili wananchi waweze kuzielewa kwa kina.

“Hapa kuna wasanii wenye vipaji vikubwa sana hivyo kama itampendeza Rais Samia ,kule anakokwenda kwa ajili ya ziara zake za kikazi kabla ya mkutano kuanza wasanii hawa waweze kutoa burudani, hivyo tunamuomba Rais na CCM kutuangalia kwa jicho la kipekee ili tuifanye kazi hiyo kwa uaminifu mkubwa,” alisema Msuya.
Zainabu Jaha ambaye ni Katibu Msaidizi amesema ikiwa watapewa nafasi hiyo watafanya vitu tofauti kupitia uigizaji, ngonjera ambazo zinazoeleza mafanikio ya Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Dkt. Samia Suluhu ikiwemo ujenzi wa reli ya kisasa, (SGR)

Pia ujenzi wa Zahanati nchi nzima ambazo kwa njia moja au nyingine zimepunguza vifo vya mama wajawazito na kuweka salama maisha ya kundi hilo wakati wa kujifungua na ujenzi wa Bwawa la kufua Umeme la Mwalimu Nyerere.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news