IRINGA-Kamati ya kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) chini ya mwenyekiti wake Mhe. Halima Mdee imeielekeza Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa kuimarisha usimamizi na kufanya ufatiliaji wa miradi yote inayotekelezwa katika Mkoa wa huo.
Maelekezo hayo yametolewa katika kikao cha majumuisho baada ya Kamati hiyo kufanya ziara ya kukagua miradi ya maendeleo katika Halmashauri hiyo na Mjumbe wa Kamati hiyo ambaye Mbunge wa Nzega Vijijini, Mhe. Dr Hamis Kigwangalla kwa niaba ya Mwenyekiti wa LAAC, Halima Mdee.
“Ofisi ya Mkuu wa Mkoa iimarishe usimamizi na kufanya ufatiliaji wa mara Kwa mara kwa miradi yote inayotekelezwa katika Halmashauri zote za Mkoa Iringa.”
Amesema, usimamizi huu ufanyike katika hatua zote za utekelezaji wa miradi ili kubaini dosari zinazoweza kuondoa thamani ya fedha na kuchukua hatua stahiki.