Mabaharia wanne wapotea Ziwa Tanganyika

KIGOMA-Mabaharia wanne wa boti ndogo za Uvuvi wamepotea katika Ziwa Tanganyika mkoani Kigoma baada ya boti zao kuzama katika ziwa hilo.
Hayo yamebanishwa na Mwenyekiti wa Chama cha Mabaharia Kanda ya Magharibi inayohusisha mikoa ya Kigoma,Katavi na Rukwa (TASU),Issa Mussa wakati wa kikao kilichohusisha Wamiliki na Wasafirishaji wa Vyombo vidogo vidogo kwa njia ya maji pamoja Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) kilichokuwa kinahusu kutoa elimu juu ya matumizi ya vifaa okozi wanapokuwa wanaendesha shughuli zao majini.

Mwenyekiti huyo amesema kuwa,tukio la kuzama Mabaharia hao limetokea Machi 2, mwaka huu ambapo boti tatu zilizama katika ziwa hilo na mpaka leo hawajaonekana na hawajulikani walipo.

Aidha, amesema siku tukio lilipotokea kulikuwa na upepo mkali ambapo hakukutakiwa mvuvi ama chombo chochote kuingizwa ziwani, lakini inaonekana wenzao walipeleka vyombo hivyo ziwani ambapo mpaka leo hawajulikani walipo na bado juhudi kuwatafuta Mabaharia hao zinaendelea.

Hata hivyo, ameiomba Serikali kupitia TASAC, kujenga Vituo vya Mawasiliano Vinavyosaidia kutoa taarifa wakati wa ajali wakiwa Ziwani, ili kurahisha kutoa taarifa na kupata msaada kwa wakati na kuepusha maafa ambayo yamepeleka watu wengi kupoteza maisha na wengine kupotea kabisa.

Kwa upande wake Afisa Mfawidhi wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC),Adam Mamilo amewataka wamiliki wa vyombo hivyo kufuata sheria za majini ikiwemo kutopakia abiria na mizigo kupita kiasi.

Vilevile kufuata utabiri wa hali ya hewa unaotolewa kila siku na Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA).

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news