LILONGWE-Baraza la Kitaifa la Elimu ya Juu nchini Malawi (NCHE) limepiga marufuku wapokeaji wa Shahada za Udaktari au Uprofesa wa heshima kutumia vyeo vya Daktari au Profesa.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na baraza hilo,tuzo hizo ni za heshima tu na hazipaswi kueleweka vibaya kama ni sifa za kitaaluma.
Baraza limeeleza kuwa,wenye udaktari wa heshima hawapaswi kujitambulisha kama madaktari kwa maandishi au hotuba badala yake wanaweza kuorodhesha jina la heshima chini ya mafanikio na tuzo kwenye wasifu wa kazi zao.