Mafanikio ya ukuaji wa uchumi wa Tanzania yanatokana na usimamizi mzuri wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT)-Rais Dkt.Mwinyi

ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Dkt. Hussein Ali Mwinyi amesema, mafanikio ya ukuaji wa uchumi wa Tanzania unatokana na usimamizii mzuri wa ichumi unaofanywa na Benki Kuu ya Tanzania (BoT).
Rais Dkt.Mwinyi ameeleza hayo alipojumuika katika Futari ya Pamoja iliyoandaliwa na benki hiyo katika Hoteli ya Madinat Tul Bahari.
Dkt.Mwinyi amesema, amekuwa akifarijika na Ushauri wa Kifedha anaoupata kutoka Benki Kuu katika kusimamia Uchumi wa Zanzibar.

Amebainisha kuwa,  mafanikio makubwa yanayopatikana hivi sasa kwa Uchumi wa Tanzania ikiwemo Zanzibar yamechangiwa na uimara wa usimamizi bora wa kifedha unaotekelezwa na BoT.
Rais Dkt.Mwinyi ameipongeza BoT kwa kuendeleza utaratibu wa kuwakutanisha pamoja wadau wa benki hiyo kila mwaka wakati wa Mwezi wa Ramadhani.

Naye Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Emmanuel Mpawe Tutuba amemuhakikishia Rais Dkt, Mwinyi kuwa, Uchumi wa Tanzania uko vizuri na unaendelea kukua na Sekta ya Fedha inafanya vizuri na mfumuko wa bei upo mdogo. .
Amesema kuwa, Uchumi wa Tanzania Bara umekuwa kwa asilimia 5.4 na Zanzibar umekuwa kwa asilimia 7.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news