ZANZIBAR-Mke wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini Zanzibar Maisha Bora Foundation (ZMBF), Mhe.Mama Mariam Mwinyi amesisitiza dhamira yake ya kuwawezesha wakulima wa mwani hususani wanawake.

Ni kwa kuhakikisha ubora wa mwani unaboreshwa, maisha yao yanaimarika na mchango wao katika uchumi wa Taifa unakua.
Mama Mariam Mwinyi amesema hayo leo alipokabidhi Makaushio ya kisasa yanayotumia nishati ya jua kwa wakulima wa mwani huko Kiuyu, Kaskazini Pemba.
Aidha, Mariam Mwinyi ametoa wito kwa wadau kuendelea kusaidia sekta ya mwani kwa uwezeshaji wa wanawake kupitia uwekezaji katika miundombinu bora, mafunzo na masoko ya uhakika, kilimo cha mwani kinaweza kuwa kichocheo kikubwa cha maendeleo ya kiuchumi.
Halikadhalika, alieleza kuwa Zanzibar Maisha Bora Foundation (ZMBF) tayari ina zaidi ya wanufaika 1,400 na inaendelea na juhudi za kuwapatia fursa zaidi kupitia miundombinu bora, mafunzo na masoko.
Tags
Dkt.Hussein Ali Mwinyi
Habari
Mama Mariam Mwinyi
Zanzibar Maisha Bora Foundation (ZMBF)
Zanzibar News